Monday, November 9, 2015


kwa mahitaji ya ramani za nyumba za kisasa kwa bei nafuu, follow instagram page @piaratz

Saturday, October 10, 2015

Ahaaaa......kumbe ni wiki mbili tu zimesalia kwa watanzania wenye sifa za kupiga kura watimize hilo jukumu lao la muhimu kikatiba...
Nimejitahidi kuzikumbukuka sifa za mtu kupiga kura ambazo zilitumika pia wakati wa uandikishwaji wa wapiga kura nimehisi inawezekana pia kuelekea siku ya upigaji kura kuna watu bado hawaelewi maana ya zile sifa za mpiga kura,
Labda tuzipitie kwa ufupi na kwa mawazo yangu ya kitanzania tena kama mtanzania wa kawaida tujaribu kujipima kama tuna sifa au bado wakosa sifa ndio watakaoamua hatma ya nchi hii?
wanasema MAADAM;
1.Una akili timamu
2.Ni raia wa Tanzania na
3.Una umri zaid ya miaka 18, basi una sifa za kupiga kura.....
Lakin wasiwasi wangu kuelekea tar.25oct.....inawezekana tukawa na watanzania wengi wakawa wanakosa mojawapo ya sifa hizo na matokeo yake ni kuipeleka Tanzania katika miaka mingine mitano ya taabu na majuto....
KWAKUWA;
-ni kwa watu WASIO NA AKILI TIMAMU TU; watakubali kuchagua viongozi wasio na uwezo eti kwa sababu tu yupo chama flan ambacho wao wanakipenda
-ni kwa WASIO NA AKILI TIMAMU TU; watakuwa tayari kujidanganya mbwa mwitu waliowadhuru miaka mitano iliyopita leo watakuwa ni rafiki zao na wataishi nao kwa miaka mingine mitano kwa amani
-ni kwa WASIO NA AKILI TIMAMU TU; watakuwa tayari kuamin kuwa viatu walivyovivua wakati wanaingia chumbani vitakuwa ni vipya pindi wakivivaa wakati wa kutoka.
KWA KUWA;
ni kwa WASIOKUWA NA MIAKA KUMI NA NANE tu wanaweza kuruhusu akili na mawazo yao yawaze baada ya wengine kuwawazia
KWA KUWA ni kwa WASIO WATANZANIA TU; watakuwa tayari kuwakabidhi nchi yao wanayoipenda watu wasio na mapenzi na nchi hii hata kwa 1%
kwa maana nyingine inawezekana WATANZANIA tunasahau
"UJINGA NI KUFANYA JAMBO LILE LILE KWA NAMNA ILE ILE KISHA UKISUBIRI MATOKEO TOFAUTI"
LAKINI; kama ww ni mmoja wapo wa watu wanaoona mapungufu katika mfumo flani lakini hutaki kuona huo mfumo ukibadilishwa inawezekana ongezeko la wasiokuwa na akili timamu litaanzaia kwako....maana tunasubiri kuona wasio na akili timamu wengine kama tulivyozoea kuwaona miaka yote.....yaani tar 25 unampa kura mgombea flani then baada ya miaka miwili unaanza kumlaani ila unapofika uchaguzi tena unasahau yote.....
TANZANIA MALI YETU SOTE.......